Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Wahudumu wa Afya ya Jamii

Jukwaa hili maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya kujiendeleza kwa njia ya mtandao maalumu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Moduli ya Kwanza: Misingi ya Elimu ya Afya kwa Mhudumu wa Afya ya Jamii

Moduli ya Kwanza: Misingi ya Elimu ya Afya kwa Mhudumu wa Afya ya Jamii

Lengo la Moduli hii ni kumjengea uwezo Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya masuala ya msingi katika kuelimisha na kuhamasisha jamii na hatimaye kuboresha afya zao. Moduli hii ina Moduli ndogo ndogo zipatazo sita.
Moduli ya Pili: Misingi ya Huduma za Uzazi, Mama na Mtoto kwa Mhudumu wa Afya ya Jamii

Moduli ya Pili: Misingi ya Huduma za Uzazi, Mama na Mtoto kwa Mhudumu wa Afya ya Jamii

Moduli hii inalenga katika kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii katika kuelimisha na kuhamasisha jamii ili waweze kupata huduma za afya na uzazi katika vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na mtoto. Moduli hii ndani yake kuna Moduli ndogo ndogo tano.

Modli ya Tatu: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii

Modli ya Tatu: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii

Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya magonjwa ya kuambukizwa na jinsi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi katika jamii. Hali kadhalika, Moduli hii ina Moduli ndogo ndogo saba.

Moduli ya Nne:  Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Yasiyoambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii

Moduli ya Nne: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Yasiyoambukizwa kwa Wahudumu wa Afya ya Jamii

Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya magonjwa yasiyoambukizwa na jinsi ya kuzuia na kudhibiti katika jamii. Ndani ya Moduli hii, kuna Moduli ndogo ndogo nne.

Moduli ya Tano: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Utapiamlo katika Jamii

Moduli ya Tano: Misingi ya Kuzuia na Kudhibiti Utapiamlo katika Jamii

Moduli hii inalenga kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii juu ya utapiamlo na jinsi ya kuzuia na kudhibiti tatizo hilo katika jamii. Moduli hii ndani yake ina Moduli ndogo ndogo nne.

Edit Page

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#