Wawezeshaji ni wataalamu waliopata mafunzo maalumu ya ujengeaji uwezo na kutambuliwa na Wizara. Wawezeshaji hawa wamejengewa uwezo na mbinu za uwezeshaji kwa Waratibu, Wataalamu wa Afya, Wahudumu wa Afya ya Jamii au Jamii kwa ujumla ili kuboresha uelewa na hamasa juu ya mambo mbalimbali ya Afya. Wawezeshaji hawa wanatumia miongozo na nyenzo zilizopitishwa na kuidhinishwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yao.
Wawezeshaji
Uwezeshaji kwa waratibu
1. Moduli na Zana za Uwezeshaji
Wawezeshaji wa Waratibu watatumia moduli za aina tatu. Moduli hizo ni;
- Moduli ya Uwezeshaji Elimu ya Afya,
- Moduli ya Uwezeshaji Huduma za Afya Ngazi ya Jamii
- Moduli ya Uwezeshaji Huduma za Afya Shuleni
Pamoja na Moduli hizi, wawezeshaji hawa pia watatumia zana mbalimbali ili kuwajengea uwezo waratibu hawa katika kutekeleza majukumu yao. Zana hizo zitajumuisha;
- Vitabu
- Miongozo
- Fomu mbalimbali
- Projector
- Manuals
- Laptop
2. Mbinu na Njia za Uwezeshaji
Uwezeshaji wa kuwajengea uwezo Waratibu utazingatia mbinu na njia za mawasilisho, mijadala, mazoezi, matembezi na maigizo.
3. Tathmini ya Maendeleo ya Uwezeshaji
Tathmini ya maendeleo ya uwezeshaji kwa Waratibu utazingatia mazoezi, mitihani, majaribio, maswali na majibu ya papo kwa hapo.
Uwezeshaji kwa wahudumu wa afya ya jamii