Jukwaa la Mawasiliano kuhusu/ya Afya
Jukwaa hili limeanzishwa ili kuwezesha elimu, taarifa na mafunzo ya afya ya umma kuwafikia wananchi na watoa huduma katika Jamii kwa urahisi na haraka zaidi. Jukwaa linajumuisha mfumo wa kimtandao (Web-based), programu za simu za kimtandao (App) na ujumbe wa kawaida (sms gateway). Lengo ni:
- Wananchi wengi kufikiwa na elimu ya afya kwa urahisi na kwa mkupuo
- Wananchi kupata fursa ya kushiriki katika mijadala inayohusu afya na huduma za afya.
- Wizara kuwajengea uwezo (mafunzo kwa njia ya kidijitali) watoa huduma ngazi ya Jamii.
- Kuwezesha mwitikio wa jamii na watoa huduma wakati kwa magonjwa ya mlipuko.
- Kuwezesha majadiliano kwa ajili ya wataalamu wa afya kwa lengo la kujengeana uwezo.