Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Vipi ni viungo vinavyotengeneza chanjo? 

Chanjo zinajumuisha vipande vidogovidogo vya vijiumbe vinavyosababisha magonjwa au chembechembe zinazounda vipande hivyo vidogovidogo. Pia zina viungo vingine vya kusaidia chanjo kuwa na ufanisi na kuwa salama. Viungo hivi vinajumuishwa katika chanjo nyingi na vimekuwa kuwa vikitumika kwa miongo kadhaa katika mabilioni ya dozi za chanjo. 

Kila kiungo cha chanjo hutumika kwa kusudi maalum na kila kiungo hujaribiwa katika mhakato wa utengenezaji na viungo vyote hufanyiwa majaribio kwa sababu za usalama. 

Utafiti katika kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona na wataalamu wa chuo cha Oxford
University of Oxford/John Cairns
Utafiti katika kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona na wataalamu wa chuo cha Oxford

Antigeni 

Kila chanjo ina kitu kinachoitwa antigeni ambacho husaidia kinga ya mwili kufanyakazi dhidi ya magonjwa na antigeni inaweza kuwa ni sehemu ndogo ya vijiumbe vinavyosababisha magonjwa (Bakteria, Virusi, pollen) kama vile protini au sukari, au inaweza kuwa ni kijiumbe kizima katika muundo ambao umedhoofika au haufanyikazi. 

Vihifadhi 

Vihifadhi huzuia chanjo kutoharibika au kuchafuliwa mara baada ya kufunguliwa kizibo au kifuniko kama itatumika kuchanja mtu Zaidi ya mmoja. 

Chanjo zingine hazina vihifadhi kwa sababu zinawekwa kwenye kasha ya dozi au kipimo kimoja kwa ajili ya mtu mmoja na kasha hutupwa baada kipimo hicho kimoja cha chanjo kutumika. 

Kihifadhi kinachotumika sana ni 2-phenoxyethanol na imekuwa ikitumika kwa miaka mingi katika chanjo kadhaa, imekuwa ikitumika katika bidhaa mbalimbali za Watoto n ani salama kutumika katika chanjo kwani sumu yake kwa binadamu ni ndogo sana. 

Chuo cha Oxford kilitangaza kwamba wanasayansi wamebuni chanjo dhidi ya COVID-19.
University of Oxford/John Cairns
Chuo cha Oxford kilitangaza kwamba wanasayansi wamebuni chanjo dhidi ya COVID-19.

Vidhibiti 

Vidhibiti huzuia athari za kemikali kutokea ndani ya chanjo na vinafanya sehemu ya chanjo hiyo kutoshikamana na makasha ya chanjo hiyo na vifuniko. 

Vidhibiti vinaweza kuwa ni sukari (lactose, sucrose), tindikali ya amino(glycine) nap rotini ya kwenye mwili wa binadamu inayotokana na hamira au chachu. 

Surfactants 

Surfactants au chembe mtungo inaweka vioungo vyote kwenye chanjo Pamoja. zinasaidia na kutulia na kutogongana kwa vitu ambavyo viko katika mfumo wa maji wa chanjo pia mara nyingi hutumika katika vyakula kama barafu. (ice cream) 

Mabaki 

Mabaki ni kiasi kidogo cha vitu anuai ambavyo vinatumika wakati wa utengenezaji au uzalishaji wa chanjo ambazo sio viungo hai katika chanjo iliyokamilishwa. Vitu vinatofautiana kulingana na mchakato wa utengenezaji uliotumiwa na vinaweza kujumuisha protini za mayai, hamira au viuatilifu. 

Athari za mabaki ya vitu hivi ambavyo vinaweza kuwapo kwenye chanjo ni ndogo sana. 

Kampuni za dawa na taasisi za utafiti wote mstari wa mbele kupata chanjo dhidi ya COVID-19.
BioNTech
Kampuni za dawa na taasisi za utafiti wote mstari wa mbele kupata chanjo dhidi ya COVID-19.

Diluent-kimiminika 

Kimiminika ni ni maji yanayotumika kulainisha chanjo kuwa katika hali sahihi inayohitajika mara moja kabla ya matumizi. Kimiminika kinachotumiwa zaidi ni maji safi. 

Adjuvant-visaidizi 

Baadhi ya chanjo zinakuwa na visaidizi. Visaidizi vinaimarisha kinga ya kuhimili chanjo, wakati mwingine kuweza kuifanya sindani ya chanjo ikae inapochomwa kwa muda mrefu au kwa kuamsha chembechembe za kinga. 

Visaidizi hivyo vinaweza kuwa ni kiwango kidogo cha chumvi kama vile  (like aluminium phosphate, aluminium hydroxide au potassium aluminium sulphate). Aluminium imedhihirisha kutosababisha matatizo yoyote ya muda mrefu ya kiafya na binadamu wamekuwa wakijipa kiwango cha aluminium kwa kula na kunywa. 

Chanjo dhidi ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na chuo cha Oxford.
University of Oxford/John Cairns
Chanjo dhidi ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na chuo cha Oxford.

Chanjo zinatengenezwaje? 

Chanjo nyingi zimekuwa zikitumika kwa miongo sasa na mamilioni ya watu wamekuwa wakipatiwa chanjo hizo salama kila mwaka. Kama ilivyo kwa dawa zote kila chanjo lazima ipitie majaribio ya kina ili kuhakikisha ni salama kabla haijaanza kutolewa kwenye program za nchi za chanjo. 

Kila chancjo ambayo inatengenezwa lazima kwanza ifanyiwe uchunguzi na tathimini ili kubaini ni antigen gani inapaswa kutumika ili kuamsha kinga. 

Awamu hii ya awali hufanyika bila kujaribiwa kwa binadamu. 

Chanjo ya majaribio hujaribiwa kwanza kwa wanyama ili kutathimini usalama wake na uwezo wake wa kuzuia magonjwa. 

Ikiwa chanjo inaleta mwitikio wa kinga , basi hapo hujaribiwa kwa binadamu katika awamu tatu. 

Awamu ya 1 

Chanjo hutolewa kwa idadi ndogo ya watu waliojitolea kutathimini usalama wake, kuthibitisha kuwa inatoa hakikisho la kinga na kuamua kipimo sahihi. Kwa ujumla katika awamu hii chanjo zinajaribiwa kwa vijana, watu wazima wenye afya njema waliojitolea. 

Majaribio ya  chanjo na Pfizer na BioNtech kwa ajili ya kupata chanjo dhidi ya COVID-19
BioNTech
Majaribio ya chanjo na Pfizer na BioNtech kwa ajili ya kupata chanjo dhidi ya COVID-19

Awamu ya 2 

Katika awamu hii chanjo hutolewa kwa mamia kadhaa ya watu waliojitolea ili kutathimini zaidi usalama wake na uwezo wake wa kujenga kinga. 

Washiriki katika awamu hii wanakuwa na sifa sawa (kama vile umri, jinsia)  kama ilivyo kwa watu waliokusudiwa. Na kwa kawaida kuna majaribio mengi katika awamu hii kutathimini makundi ya umri mbalimbali na michanganyiko tofauti ya chanjo. 

Kundi ambalo halikupata chanjo kwa kawaida hujumuishwa katika awamu kama kikundi cha kulinganisha ili kubaini ikiwa mabadiliko katika kikundi kilichochanjwa yametokana na chanjo au yametokea kwa bahati. 

Pfizer na BioNTech wasema chanjo waliobuni ina uwezo wa kuzuia COVID-19 kwa asilimia 90.
BioNTech
Pfizer na BioNTech wasema chanjo waliobuni ina uwezo wa kuzuia COVID-19 kwa asilimia 90.

Awamu ya 3 

Katika awamu hii chanjo hupewa maelfu ya watu waliojitolea huku wakilinganishwa na kundi kama hilo la wale ambao hawakupata chanjo lAkini walipokea bidhaa za kulinganisha, kubaini ikiwa chanjo hiyo ni bora dhidi ya ugonjwa ambao imeteundwa kulinda dhidi yake na kubaini usalama wake katika kundi kubwa la watu. 

Majaribio mengine ya awamu ya tatu hufanywa katika nchi nyingi na sehemu nyingi ndani ya nchi ili kuwa na uhakika wa utendaji wa chanjo hiyo unaonekana kwa watu wengi tofauti. 

Wakati wa majaribio ya awamu ya pili nay a tatu waliojitolea na wanasayansi wanaoendesha utafiti huwa wanafichwa kujua ni kina nani waliopewa chanjo au waliopokea bidhaa za kulinganisha. Hii inaitwa “kupofusha” na inapaswa kuhakikishwa kuwa waliojitolea au wanasanyansi wanaofanya utafiti hawaathiriwi katika tathimini yao ya usalama au ufanisi wa kujua ni nani aliye na bidhaa gani. 

Baada ya majaribio kumalizika na matokeo yote kukamilika waliojitolea na wanasayansi walioendesha majaribio wanaarifiwa ni nani aliyepata chanjo hiyo n ani nani aliyepewa bidhaa za kulingana. 

Wakati matokeo yote ya majaribio haya ya kliniki yanapopatikana hatua kadhaa zinahitajika zikiwemo tathimini ya uhakiki wa ufanisi na usalama kwa idhini ya ya sera za afya ya umma. 

Maafisa katika kila nchi hutathimini kwa kina takwimu za majaribio na kuamua endapo waidhinishe chanjo hiyo kwa matumizi. 

Chanjo lazima ithibitishwe kuwa salama na yenye ufanisi kwa idadi kubwa ya watu kabla ya kuidhinishwa na kuingizwa kwenye programu za kitaifa  za chanjo.  

Kizuizi cha usalama na ufanisi wa chanjo ni kikubwa sana , kwa kutambua kwamba chanjo hupewa watu ambao wana afya njema na haswa ambao hawana maradhi au sio wagonjwa. 

Ufuatiliaji zaidi unafanyika kwa njia ya kuendelea baada ya chanjo kutolewa. Kuna mifumo ya kufuatilia usalama na ufanisi wa chanjo zote. 

Hii inawawezesha wanasayansi kufuatilia athari za chanjo na usalama hata kama zinatumiwa kwa idadi kubwa ya watu kwa muda mfrefu. 

Takwimu hizi hutumiwa kurekebisha sera za matumizi ya chanjo ili kuongeza athari nzuri za chanjo hizo na pia kuruhusu chanjo hiyo kufuatiliwa kwa usalama kupitia wakati wote wa matumizi yake. 

Wakati chanjo inapoanza kutumika ni lazima ifuatiliwe kila wakati ili kuhakikisha inaendelea kuwa salama. 

Matukio Maarufu

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#