Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

                                                                                                                                                                                                                                                  

Na WAF- Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameweka wazi kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya imesaini hati za makubaliano saba (7) kwaajili ya mashirikiano ya kimataifa katika kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Prof. Makubi amesema hayo leo katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, tukio lililoambatana na usainiaji wa Mkataba wa saba na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Alameda Bw. Neeraj Mishra iliyopo nchini Misri na kuhudhuriwa na Waandishi wa habari.

Ametaja, Hospitali zilizo katika makubaliano hayo ni pamoja na Hospitali ya MIOT ya nchini India, Hospitali ya Sheba ya nchini Israel, pamoja na nchi za Uturuki, Kenya, Burundi, Rwanda na Hospitali ya ALAMEDA iliyo nchini Misri.

Aidha, Prof. Makubi ameweka wazi kuwa, hati hizo za makubaliano zimelenga kuimarisha mahusiano katika mafunzo kwa watumishi wa afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi ambapo zaidi ya Wataalamu 20 hufaidika kila mwaka kwa gharama nafuu.

Ameendelea kusema kuwa, makubaliano hayo yamelenga kubadilishana Wataalamu ambapo watapata fursa ya kwenda kujifunza nje ya nchi, pia Wataalamu wa nje kuja kufanya kazi na Wataalamu wetu wa ndani ya nchi.

Pia makubaliano hayo yamelenga mashirikiano ya kikanda katika masuala ya udhibiti wa magonjwa ya dharura mipakani, masuala ya tafiti za tiba na kinga, huduma za tiba mtandao na Tehama, pamoja na viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Mwisho 

Matukio Maarufu

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#