Uhakiki wa Vielelezo
Huu ni ukurasa maalumu unaokuwezesha kupata huduma ya upitiaji, uhakiki na uidhinishaji wa matumizi ya vielelezo mbalimbali vinavyokusudiwa kuielimisha, kuihamasisha au kuishirikisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya Afya. Kupitia eneo hili utafahamishwa juu ya ratiba ya uhakiki kwa mwaka mzima, utaratibu wa Kamati ya Uhakiki wa Vielelezo vya Elimu ya Afya kwa Umma, mwongozo na utaratibu wa uandaaji wa Vielelezo kuanzia hatua za awali mpaka usambazaji, pamoja na vigezo vyote vya kuzingatia ikiwemo viambatisho wakati wa kutuma maombi ya uhakiki. Kuhusu uhakiki zingatia kalenda hapa kulia.