Wizara ya Afya

JUKWAA LA KIDIJITALI LA ELIMU YA AFYA KWA UMMA

Afya Yangu, Mtaji Wangu

Wizara ya Afya

Huduma za Afya Shuleni

Checked Out

Utangulizi

Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Shuleni unajumuisha mikakati, shughuli na huduma zinazolenga kudumisha afya bora ya watoto na kuchangia mafanikio katika masomo yao.

Dira

Jamii yenye afya na ustawi bora ambao utachangia maendeleo ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa.

Dhamira

Kuhamasisha, kulinda na kurejesha afya na ustawi wa wanafunzi na jamii zao kwa kuhakikisha  huduma za afya zinapangwa, zinasimamiwa na kutolewa kwa ufanisi  ili kufikia maendeleo endelevu ya afya na elimu.

Malengo

Kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Shuleni.
Kuimarisha mfumo wa uongozi ndani ya Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Shuleni
Kuimarisha utekelezaji wa afua jumuishi kupitia shule
Hakikisha uratibu ushirikiano na utendaji mzuri katika utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Elimu ya Afya Shuleni.
Kufuatilia upatikanaji, ugawaji na matumizi sahihi ya rasilimali
Kuhakikisha utafiti wa utendaji, ufuatiliaji, tathmini na usimamizi wa huduma za Elimu ya Afya Shuleni
Kuweka daraja kati ya Afya na Elimu kuahikiksha malengo ya Elimu ya msingi yanafikiwa

Uniti

Majukumu ya Uniti ya Chekechea
  • Kusimamia uelimishaji na uhamasishaji wa masuala ya afya kwa watoto wa chekechea.
Majukumu ya Uniti ya Msingi
  • Kusimamia uelimishaji na uhamasishaji wa masuala ya afya kwa wanafunzi wa elimu ya msingi.
Majukumu ya Uniti ya Sekondari
  • Kusimamia uelimishaji na uhamasishaji wa masuala ya afya kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari.
Majukumu ya Uniti ya Chuo
  • Kusimamia uelimishaji na uhamasishaji wa masuala ya afya vyuoni.

Muundo

Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Shuleni-WAMJW

Mratibu wa Huduma za Afya Shuleni -OR-TAMISEMI

Mratibu wa Huduma za Afya Shuleni-Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Mratibu wa Health Promotion Mkoa - Sekta ya Afya

Mratibu wa Huduma za Afya Shuleni - Sekta ya Elimu

Mratibu wa Health Promotion Halmashauri - Sekta ya Afya

Mratibu wa Huduma za Afya Shuleni - Sekta ya Elimu

Nyaraka za Huduma za Afya Shuleni

WASILIANA NASI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Wizara ya Afya

Mji wa Serikali - Mtumba,

S.L.P. 743,

40478 DODOMA.

+255-22-2342000/5

ps@afya.go.tz

Call Center: 199 | *199#